
Mad Ice kuwashika
Friday, 24th Feb, 2012
Mwanamuziki Mad Ice ameiambia Enewz kuwa yeye pamoja na mtayarishaji wa muziki Miikka Mwamba wapo katika hatua za mwisho za upikaji wa kazi mpya ambayo itawashika mashabiki vilivyo pindi itakapotoka.
Mad Ice amesema kuwa kazi hii itakuwa ya tofauti na zile watu walizozoea kutoka kwake kwa hivyo mashabiki wakae tayari kuipokea, na hakutaka kuisemea zaidi kazi hii.
Ngoma ya 'Mapenzi Sumu' ndiyo inayofanya vizuri kwa sasa kutoka kwa Mad Ice ambapo pia msanii huyu ana albam Extended Play yenye nyimbo kumi inayokwenda kwa jina 'Maisha'.
No comments:
Post a Comment