Mwanadada Stella mwangi amesema kuwa hana tatizo na jitihada zilizokuwa zimechukuliwa na kamati ya mazishi ya baba yake kuchangisha fedha kwa ajili ya gharama za msiba wa baba yake huko Kenya.
Stella amesema kuwa ana heshimu hatua hiyo ikiwa ni moja ya ishara kuwa baba yake alikuwa ni mtu anayetambulika na kuheshimiwa lakini kile kilichomkera ni ile hatua ya wanakamati kutumia jina lake katika kutafuta mchango, na kuleta picha kwamba yeye ameshindwa kumudu kugharamia msiba huo wa baba yake kipenzi.
Mwanadada huyu ambaye anafanya vizuri katika muziki ameongea haya katika kujibu tuhuma za moja mwanakamati aliyekuwa akisimamia zoezi la kuchanga fedha, akisema kuwa STL pamoja na mama yake wamesusia zoezi hilo la mchango.
Jeff Mwangi amelazwa katika makazi yake ya milele huko Murang'a siku ya Jumamosi.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, ameen.
No comments:
Post a Comment